TANGAZA NASI

Kiatu Media

Feedjit

Tuesday, July 9, 2013

"BONGE LA BWANA!" YA HASHIM SAIDI AU "MZEE WA MAJANGA" WA MASHAUZI CLASSIC...


Muimbaji wa bendi ya Mashauzi Classic ya jijini Dar, Hashim Saidi maarufu kama mzee wa Majanga, amerokodi wimbo uitwao "Bonge la bwana".

Mzee wa Majanga ameuambia mtandao wa Taarabuzetu.blogspot.com kuwa, wimbo huo anatarajia kuuachia rasmi ndani ya mwezi wa Ramadhani, katika albam iliyopita pia Hashim saidi alirekodi wimbo uitwao "Niacheni nimpende" akiwa na bendi hiyo ya Mashauzi Classic chini yake Mkurugenzi Isha mashauzi.

Akiuzungumzia zaidi wimbo wake huo mpya alisema ni wimbo unaomzungumzia mwanaume anaejiamini na hateteleki kwa chochote kile.
Amewaomba wadau kuendelea kumuunga mkono kama walivyofanya ktk wimbo wake uliopita. Huyo ndio Hashim Saidi mzee wa Majanga au Rais wa Mamaa Fatu China!!.