TANGAZA NASI

Kiatu Media

Feedjit

Monday, July 8, 2013

AT AJA NA NYIMBO MPYA "KITUMBUA"...!

Msanii maarufu wa miondoko ya mduara AT amerekodi nyimbo yake mpya iitwayo "Kitumbua" akizungumza na Taarabuzetu.blogspot.com msanii huyo amesema kitumbua ni nyimbo nzuri ambayo anaamini itawapa burudani nzuri wadau na mashabiki zake, ameendelea kwa kuwaomba mashabiki zake kumpa sapoti kubwa katika kuichagua nyimbo kwenye vituo vya redio na television pindi atakapoiachia.

AT amesema katikati ya wiki hii ataiachia nyimbo hiyo ili wadau na mashabiki waisikie na kuiona kwa umakini zaidi, anamalizia kwa kujitamba kwamba mara zote huwa habahatishi anapoachia track yoyote...
Huyo ndio AT!. Kaa mkao wa kusubiri pindi nyimbo itakapotoka utaipata hapahapa Taarabuzetu.blogspot.com