TANGAZA NASI

Kiatu Media

Feedjit

Sunday, July 14, 2013

ALBAM YA "DOMO LA UDAKU" YA T MOTTO MODERN TAARAB YAUZWA MITAANI KINYEMELA!!

T Moto Modern Taarabu
Albam mpya ya T MOTTO MODERN TAARAB, wajanja wameanza kuiuza mitaani hata kabla uongozi wa bendi hiyo haujaanza kufanya hivyo.

Albam hiyo ambayo ina nyimbo tano:-
1. Domo la Udaku muimbaji "Jokha kasim",
2. Behind the scene muimbaji "Nyawana Fundikila",
3. Wewe si daktari wa mapenzi muimbaji "Nassoro Hussein"
4. Mwanamke hashuo muimbaji "Shinuna Kasimu" na
5. Ubaya una mwisho muimbaji Aisha Masanja.

Mkurugenzi wa T Moto, Amini Salmini (kushoto) na muimbaji wa kundi hilo, Jokha Kassim
Mnyetishaji wa habari hizi aliuambia mtandao wa taarabuzetu.blogspot.com kwamba "AUDIO CD" za Albam hiyo zimekuwa zikiuzwa kwa wingi mitaa ya Yombo, Mbagala, Mwenge, Sinza na Magomeni na wauzaji wakubwa wa nyimbo hizo ni "wamachinga" wanaouza CD mikononi na baadhi ya flemu za magomeni zinazouza CD.

Sisi kama wadau, taarabuzetu.blogspot.com bado tunaendelea kutoa rai kwa Serikali kusimamia kwa dhati haki za wasanii kwani kila kukicha maharamia wamekuwa wakiongezeka. Wasanii wengi wa musiki "kama sio wote" wanalia sana na hili swala la wizi wanasema wizi hao na hata kama wakikamatwa wamekuwa hawapewi adhabu kali ili wasirudie!.

"Serikali itilie mkazo na ifuatilie kwa undani suala hili ili wezi waweze kukamawa na wapewe adhabu kali ili wasiludie na wale wenye mawazo hayo wasifanye kabisa"