TANGAZA NASI

Kiatu Media

Feedjit

Wednesday, July 10, 2013

Hammer Q Kuachia Video ya "Tunapendana".


Baada ya safari ndefu aliyoifanya na kundi lake la Offside Trick na kurejea Jijini msanii Hammer Q ataachia Video ya "Wapendanao".

Msanii maarufu na wa siku nyingi katika Gemu la muziki Tanzani ambaye ni msanii wa Kundi la Offside Trick Hammer Q, ataachia Video ya Nyimbo yake aliyoshirikiana na Mkewe Salha Abdallah wa King's Modern Taarabu.

Akizungumza na mtandao wa Taarabuzetu.blogspot.com Hammer Q alisema shooting ya nyimbo hiyo imeshakamilika na anatarajia kuiachia siku ya Ijumaa July 12.

Alitaja jina la nyimbo kuwa ni "WAPENDANAO" Ambayo Audio yake ipo inatesa kwa sasa katika vituo mbalimbali vya Radio.

Wimbo ukiwa ni ujumbe tosha kwa Yeye "Hammer" na Mkewe "Salha" kuonesha umma kuwa "Wanapendana". Anawaomba wadau wote wamsapoti kwa kumuunga mkono kwa kuipokea video hiyo.

Video imefanyika katika Studio ya Akhenaton iliyopo Kigamboni jijini Dar es Salaam.