TANGAZA NASI

Kiatu Media

Feedjit

Monday, July 29, 2013

WASANII KUMI BORA CHIPUKIZI WALIOFANYA VIZURI 2008 MPAKA 2013!!!

Muziki wa Taarabu ni muziki unaopendwa na wengi hususani Ukanda huu wa Pwani. Kila kukicha Wasanii mbalimbali chipukizi wamekuwa wakijiingiza na kufanikiwa kufanya vizuri.

Yafuatayo ni majina ya Wasanii kumi bora wanaofanya vizuri kwa sasa kupitia vituo mbalimbali vya redio kama inavyoletwa kwenu na Mtandao Makini wa taarabuzetu.blogspot.com.

1. Mwanahawa Ally. "Chipolopolo”
Alipotoka Victoria na kwenda Dar Moern Taarabu walimdharau na kumbeza, lakini hakukata Tamaa alipitia Supershine na kudondokea King’s Modern Taarabu. Hapo ndipo Nyota yake ikaanza kung’aa na kufanikiwa kurekodi nyimbo 2 Matata sana “Mchumia Juani” na “Dunia Duara”
Huyo ndio Chipolopolo anashika namba moja!

2. Nyawana Fundikila.
Mwanzoni alikuwa Solo-Artist, akafanikiwa kutoa wimbo wake uitwa “Nipo kamili nimejipanga”. Wimbo ambao ulileta matatizo makubwa baina yake na Isha Mashauzi. Hkuishia hapo akatoa wimbo mwingine uitwa “Umesharoga wangapi”. Ndipo King’s walipogundua uwezo wake na kumjumuisha katika bendi, hata hivyo hakukaa sana akatimkia T. Motto Modern Taarab ambapo alitoa wimbo mmoja uitwa “Behind the Scene” Utunzi wake mwenyewe. Huyo ndio Nyawana anshika namba mbili!

3. Hanifa Maulidi.  "Jike la Chui"
Huyu ana safari ndefu ya muziki mpaka kufikia mafanikio. Kwa kifupi amepitia Super Shine, Melody, Coast, Mashauzi mpaka King’s alipofanikiwa kutoa wimbo mwingine nje ya Bendi uitwa “Makavu live” unaotamba sana katika vituo vya redio sasa hivi. Huyo ni Hanifa Maulidi ukipenda muite Jike la Chui anashika nafasi ya Tatu!

4. Aisha Othman. "Vuvuzela”
Mwanzoni wakati yupo Dar Modern na Director wake Mlidu Ally kumuita Aisha Vuvuzela alikuwa akichukia sana. Lakini sasa limekuwa ni jina maarufu ambalo linamtambulisha katika sanaa. Vuvuzela ana sauti nzuri sana kwenye kuimba. Alipotoka Dar Modern alijiunga na Mashauzi Classic ambapo hakukaa sana na sasa hivi ni msanii wa King’s Modern Taarabu. Hivi karibuni anatarajia kutoa wimbo mpya kabisa akiwa King’s Modern Taarabu. Huyo ndie Aisha Vuvuzela anashika nafasi ya nne!

5. Abdul Malick “Handsome wa Mashauzi”
Ukimuona hutaweza kuamini kwamba aweza kua na sauti nzuri kiasi kile. Mwanzoni alipokuwa King’s Director wake Kijoka hakuwa akimpa kipaumbele sana akaenda zake Coast kwa Omary Tego ambapo hakukaa sana akahamia Mashauzi Classic na kutoa wimbo “Sintosahau kwa yaliyonikuta”. Huyo ndio Abdul Malick ukipenda muite Handsome wa Mashauzi, yeye anashika nafasi ya tano!

6. Kibibi Yahaya.
Ukimuuliza nini siri ya mafanikio yako ataanza kwa kucheka halafu atakujibu ni mazoezi na nidhamu pindi ninapokuwa kazini. Kibibi alianzia Bendi ya Supershine, alipoona ameiva kidogo akaamua kwenda Coast Modern Taarabu kwa Omary Tego ambapo alifanikiwa kurekodi wimbo mmoja na kuhamia Bendi ya King’s ambapo napo amefanikiwa kurekodi wimbo mmoja pia. Kibibi ni msanii anaetegemewa sana na uongozi wa King’s kwa sasa. Huyo ndio Kibibi anashika nafasi ya sita!

7. Salha Abdallah wa Hammer Q
Wakati anaanza kuimba mashabiki walishindwa kumtofautisha kati yake na marehemu Mariam Hamisi kipindi hicho. Kiukweli wamefanana sana! Salha alianzia Dar Modern Taarab lakini mwezi uliopita amejiunga na King’s Modern Taarabu ambao chini ya Mkurugenzi wake Hamisi Majaliwa. Salha kwa sasa ana wimbo mpya ndani ya King’s Modern Taarabu ambao anasema ni mapema sana kuutambulisha. Huyo ndio Salha Abdallah mke halali wa Hammer Q. Yeye anashika nafasi ya 7!

8. Fatuma Mcharuko. Jahazi Modern Taarabu
Anapokuwa stejini anajituma sana ili kuhamasisha wapenzi na mashabiki. Katika albam iliyopita ya Jahazi, Fatuma alipewa wimbo mmoja kuimba ambao aliutendea haki sana! wimbo huo ambao mashabiki wameubadilisha
jina na sasa wanauita “Umenipandisha Mizuka Tawile! Tawile! Tawile! ni moto wa kuotea mbali na
kila unapopigwa ni lazima watu wanyanyuke na kucheza. Huyo ndio Fatuma Mcharuko Msanii toka Jahazi
Modern Taarab anashika nafasi ya nane!

9. Saida Mashauzi.
Hana muda mrefu katika muziki wa Taarabu hapa nchini. Ila ni mdogo wake Isha Mashauzi Mkurugenzi wa
Mashauzi Classic. Ana uwezo mkubwa wa kuimba kubadilisha sauti yake kulinga na wimbo husika anaoimba wakati huo. Huyo ndio Saida Mashauzi anashika nafasi ya tisa!

10. Kapteni Temba.
Kwa sasa ndio mkurugenzi wa Fungakazi Modern Taarabu, yenye mskani yake Kigamboni Dar. Alianza kama Solo-Artist kwa kutoa nyimbo zake kadhaa, mpaka pale alipofanikiwa kufungua bendi yake ya Funga kazi.
Kw muda huu yupo studio na kundi zima la Bendi yake wakirekodi Albamu nyingine tena. Huyo ndio Kapteni Temba Mchaga wa kwanza kuimba Taarabu hapa Tanzania.

1 comments:

Anonymous said...

UMEJITAHIDI KUWATAJA KWA MAJINA ILA KWENYE NAMBA HUJUWA SAHIHI SANA MANA FATMA MAHMOUD NA SALHA ABDALLAH HAWAKO KATIKA NAMBA ZINZOSTAHILI. MWANAHAWA CHIPOLOPOLO KWELI ANAIMBA ILA HAJAFIKA STAGE YA MCHARUKO HATA KIDOGO PENYE UKWELI LAZIMA TUSEME KAMA WADAU.

Post a Comment