TANGAZA NASI

Kiatu Media

Feedjit

Tuesday, July 9, 2013

KING'S MODERN TAARAB KUTENGENEZA NYIMBO 2 MPYA KALI



Bendi inayokuja kwa kasi kwa sasa, King's Modern Taarab inatarajia kutengeneza nyimbo 2 kali wakati wa mapumziko ya mfungo wa Ramadhani.
Salha Abdallah
Akizungumza na mtandao wa taarabuzetu.blogspot.com Director mkuu wa bendi hiyo "Alhaji Kijoka" alisema wamejipanga vyema kuingia katika soko la ushindani kwa style yake, kuna nyimbo 2 za wasanii wetu wapya zitatengenezwa, aliwataja wasanii hao kuwa ni Aisha Vuvuzela aliyetokea Mashauzi Classic na Salha Abdallah huyu ametokea Dar Modern Taarab.

Alipoulizwa nyimbo hizo zitaitwajwe! Director Alhaji alisema hawezi kutaja majina ya nyimbo hizo kwani ni mapema sana na kuna watu wana tabia ya kuiba majina ya nyimbo yanapokuwa mazuri na kuyatumia wao. Aliwaomba wapenzi wa Taarabu nchini kutegemea nyimbo nzuri toka kwao King's Modern Taarabu baada tu ya Ramadhan kuisha.