TANGAZA NASI

Kiatu Media

Feedjit

Sunday, July 21, 2013

SIKU CHACHE BAADA YA KUUZA GARI LAKE, HADIJA KOPA AIBIWA MKOBA WAKE WA FEDHA....

Wiki iliyopita katika mtandao huu tulilipoti juu ya malkia wa taarabu bibie Hadija kopa kuuza gari lake aina ya Noah!, chakushangaza, kustaajabisha na kuhuzunisha vibaka walivizia nyumba ya malkia huyo iliyopo Bagamoyo maeneo ya Magomeni na kufungua dirisha la kioo cha dirisha la malkia huyo na kuiba mkoba ambao kwa taarifa za malkia mwenyewe kulikuwa na shilingi elfu 20/= na sio zaidi.
Unajua ndugu mwandishi hawa inaonekana wamesoma ktk mtandao wenu wakajua nina pesa ndani kwa vile nimeuza gari, kwahiyo walikuja rasmi kuziiba nyumbani, alimaza kwa kuuelezea mtandao huu wa Taarabuzetu.blogspot.com.
Sisi kama wadau na wapenzi wakubwa wa Taarabu nchini tunakupa pole sana Malkia wa mipasho.

0 comments:

Post a Comment