TANGAZA NASI

Kiatu Media

Feedjit

Thursday, July 11, 2013

AISHA VUVUZELA, THABIT ABDUL, OMARY ALLY NA RAHMA MACHUPA WAGEUKIA KASWIDA.....

Thabit Abdul

Ule msemo wa kiswahili usemao mgeni njoo mwenyeji apone umejidhihirisha kwa wasaani hawa wa Taarabu Rahma machupa wa jahazi, Aisha Vuvuzela wa King's, Omary ally wa TOT na Thabit Abdul wa 5 stars, kwa pamoja wameanza kutengeneza nyimbo za kaswida maalum kwa mfungo huu wa Ramadhani.

Director Thabit Abdul amesema wakati akiitanabaisha taarabuzetu.blogspot.com kwamba watakuwa wakifanya hivyo kila inapoingia Ramadhani kwani hii ni program endelevu.
Ameendelea kusema kwamba hivi karibuni watakwenda kuzirekodi nyimbo hizo ili kuweza kutoa mafundisho kupitia ujumbe mzuri uliopo humo.

Sisi kama uongozi na wafanyakazi wote wa mtandao makini wa taarabuzetu.blogspot.com tunawapongeza kwa hatua mliyofikia, kwani "Umoja ni Nguvu na Utengano ni Udhaifu".

RAMADHAN KAREEM!.