TANGAZA NASI

Kiatu Media

Feedjit

Friday, July 12, 2013

HASSAN VOCHA TOKA DAR MPAKA MOMBASA... BALAA!!

Hassan Vocha...
Msanii Hassan Vocha ametoa wimbo wake mpya kabisa wa mduara aliomshirikisha Nyota ndogo wa kenya.

Wimbo huo uitwao "Siwezi kulala" umerekodiwa katika Studio ya "Vibe Record ya Mombasa" .
Akiongea na mtandao wa taarabuzetu.blogspot.com Hassan Vocha alisema kwamba ameamua kumshirikisha Nyota Ndogo katika wimbo huo ili kuleta radha tofauti masikioni mwa wapenzi wa miduara.

Amewaomba wadau wampe tafu katika kuchagua wimbo wake huo. Wakati huo huo Hassan vocha ambae yupo ktk bendi ya G5 Modern Taarabu pia anatarajia pia kuuachia wimbo mwingine wenye mahadhi ya taarabu uitwao "Dont break my heart" aliouimba akiwa ndani ya bendi yake ya G5 Modern Taarabu chini ya mkurugenzi wake Hamisi Slim.
Nyota Ndogo toka Kenya.