TANGAZA NASI

Kiatu Media

Feedjit

Tuesday, July 9, 2013

BI AFUA SULEIMAN "B 52" BAADA YA KIMYA KIREFU HATIMAE AFUNGUKA.....!

Bi Afua Suleiman
Muimbaji nguli, mkongwe wa Taarabu nchini Tanzania, Bi Afua Suleiman au B52 kama anavyoitwa na mashabiki wake, amefunguka juu ya ukimya wake!.

Bi Afua ambae amepitia bendi nyingi ikiwemo East african Melody, kwa sasa ni muimbaji wa bendi ya Gusagusa min Bend ya Jijini Dar es Salaam.

Baada ya kutoa wimbo wa "Jidodo linakuchukucha" akiwa na Gusagusa min Bend, alionekana kupotea kabisa na kukaa muda mrefu pasipo kutoa wimbo wowote. Ndipo mtandao wa taarabuzetu.blogspot.com ulipomtafuta. Bi Afua amesema kwamba ana nyimbo mpya ndani ya bendi yake hiyo ambayo ataifanyia mazoezi wakati wa mwezi mtukufu wa Ramadhani, alipoulizwa jina la nyimbo ili wadau waujue alisema hawezi kutaja jina la wimbo kwani ni mapema sana, ila aliwaomba wadau na wapenzi wake kukaa mkao wa kula kwani hiyo nyimbo itakuja kuwashika haswaaaa!!

Huyo ndio Bi Afua Suleiman "B52" muimbaji mkongwe kabisa wa muziki wa Mwambao Tanzania Mnyamwezi anaejiamini daima!.