TANGAZA NASI

Kiatu Media

Feedjit

Tuesday, July 23, 2013

HADIJA KOPA, KUANZA KAZI RASMI TAR 19 MWEZI WA KUMI NA BENDI YAKE YA T.O.T.!.

 Malkia wa mipasho nchini Tanzania Hadija Omary Kopa, anatarajia kuanza tena kazi rasmi kuanzia mwezi wa kumi tarehe 19 mwaka huu 2013.

Akizungumza na mtandao makini wa taarabuzetu.blogspot.com Malkia alisema: kipindi hicho nitakuwa nimeshamaliza edda na nitaanza tena kusimama majukwaani ingawa nitakuwa katika majonzi makubwa, kwani nilizoea kuwa na mume wangu karibia kila show... leo hii nakuwa peke yangu... aah! yote namuachia mungu. Kikubwa namuomba mungu ampumzishe pema peponi mume wangu kipenzi...! alimaliza kwa kusema huku akilia machozi.

0 comments:

Post a Comment