TANGAZA NASI

Kiatu Media

Feedjit

Monday, July 8, 2013

UZINDUZI WA G5 MODERN TAARAB FUNIKA MBAYAAA!!.

G5 Modern Taarab imefanya kufuru ya mwaka baada ya kufanikiwa kufanya utambulisho wa bendi yake kwa mafanikio makubwa hapo jana ndani ya ukumbi wa Ikweta Grill Mtoni kwa Azizi Ally.

Show hiyo ambayo ilidhaminiwa na kampuni ya Mabibo wine, kupitia kinywaji chake cha Windhock lager kila mshabiki alipewa chupa moja mlangoni. Mashabiki walianza kuingia ukumbini kuanzia saa 2 usiku mpaka ilipofika saa 5 na nusu ukumbi ulikuwa umeshajaza watu.

Bendi za dansi za Extra bongo na Msondo ngoma zilisindikiza uzinduzi huo na kufanya upendeze zaidi. Wapenzi na washabiki walisikika wakisema karibuni G5 modern taarab katika ushindani wa muziki wa taarab nchini tanzania.

Mtandao huu wa Taarabuzetu.blogspot.com unawapongeza sana kwa kufanikisha uzinduzi na kuongeza idadi ya bendi za Taarabu nchini Tanzania na kufanya ushindani uwe mkubwa zaidi, tunaamini mtaleta changamoto nyingi sana za kutoa burudani.
KARIBU G5 MODERN TAARABU.