TANGAZA NASI

Kiatu Media

Feedjit

Tuesday, July 16, 2013

TETESI;- ALLY J AUVURUGA UONGOZI WA 5 STARS. YASEMEKANA KALA PESA ZA BI MWANAHAWA ALLY....

Ally J
 Msanii wa 5Stars Modern Taarabu Ally J, inasemekana amekuwa haelewani vyema na viongozi wenzake mpaka kupelekea wamuone kama mbinafsi.

Akizungumza na mtandao wa taarabuzetu.blogspot.com kiongozi mmoja wa 5Stars ambae hakupenda kutajwa jina lake alisema kwamba wamechoshwa na tabia za kiongozi mwenzao kwani amekuwa ni mtu mwenye kujiamulia mambo peke yake pasipo kuwashirikisha wenzake.

Aliongeza kuwa, Mfano zinapokuja pesa za show huwa anakata pesa yake juu kwa juu ndipo zinazobaki anawapa wenzake, huu si utaratibu tuliyojiwekea. Pia ally j alipewa pesa milioni moja na laki tano ampelekee Bi mwanahawa ally lakini yeye akampa milioni moja tu, laki tano hakumpa akaweka mfukoni mwake...! Kitu ambacho kinamfanya mpaka sasa Bi Mwanahawa haji katika show kwasababu ya pesa zake!.

Sisi kama viongozi wenzake tunamuomba abadilike ili twende sawa la sivyo nibora tubadili jina la bendi ili tuone, maana labda mwenzetu anajivunia 5 Stars yake... Alimaliza kulipa nyeti hizo muhimu dawati la mtandao huu!.

Baada ya kupata taarifa hizi mtandao huu ulimpigia simu muhusika bwana Ally J ili kuweza kupata ukweli, baada ya kumsomea tuhuma hizo alikataa kuwa hakuna kitu kama hicho katika Bendi na hawezi kamwe kufanya kitu kama hicho na akashauri apigiwe simu Mwanahawa ili aweze kuthibitisha na tuweze kupata habari zaidi.

Tumejitahidi kumtafuta Bi Mwanahawa bila mafanikio muda wote simu yake ilikuwa haipatikani. 

Sisi kama mtandao makini tunauomba uongozi wa 5Stars kukaa chini na wafanyakazi wote ili kuangalia malalamiko haya kama yanaukweli wake kabla mambo hayajaharibika zaidi.