TANGAZA NASI

Kiatu Media

Feedjit

Tuesday, July 16, 2013

SIHAMI MASHAUZI CLASSIC MPAKA INIFIE MIKONONI!! - ABDUL MALICK...!!


Abdul malick
Muimbaji wakiume wa Mashauzi Classic ambae ameimba nyimbo ya "Sintosahau kwa yaliyonikuta" Abdul Malick au "Handsome wa Mashauzi" kama anavyojulikana na mashabiki wake ameuambia mtandao wa taarabuzetu.blogspot.com kwamba hahami, hatohama na wala hatarajii kuhama katika Bendi yake ya Mashauzi Classic kwani inamjali na ina mthamini kwa kiasi ambacho hafikilii kuondoka mpaka itakapomfia mikononi mwake!.

Abdul Malick ambae kwa sasa ana nyimbo mpya ndani ya Mashauzi Classic iitwayo "Why me!" ndio msaani anaeongoza kwa kusimamishwa na uongozi kutokana na utovu wa nidhamu mara kwa mara.

Alitumia nafasi hiyo pia kuwaomba radhi viongozi, wasanii wenzake na wapenzi wa Mashauzi Classic kwa ujumla kwa yaliyokuwa yanatokea nyuma juu yake, "naahidi hayatojitokeza tena".

Huyo ndio Abdul malick au ukipenda muite Handsome wa Mashauzi Classic!!.