TANGAZA NASI

Kiatu Media

Feedjit

Monday, July 8, 2013

JAHAZI YAVUNJA JUNGU KWA KISHINDO KIKUBWA TRAVETINE MAGOMENI!!.

Jahazi modern Taarabu jana usiku ndani ya ukumbi wao wa nyumbani wa Travertine magomeni jijini Dar, walifanya onyesho lao la mwisho kabla ya kuukaribisha mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Wakitumia uzoefu wao na umakini katika kazi kama ilivyo kawaida, Jahazi waliporomosha burudani ya nguvu, walianza kwa kupiga nyimbo zao za zamani ambazo zilipendwa sana na kumalizia kwa kupiga nyimbo zilizo katika albam yao mpya iitwayo "Wasiwasi wako ndio maradhi yako".

Alipoingia mzee yusuph kuimba umati wa watu ulilipuka kwa shangwe na mayowe, yote ni kuthibitisha ni kwa kiasi gani wanamkubali mfalme mzee yusuph.

Mpaka inapigwa nyimbo ya mwisho mashabiki bado walikuwa wanaonyesha wana kiu ya burudani toka katika bendi hiyo.