TANGAZA NASI

Kiatu Media

Feedjit

Wednesday, July 10, 2013

HASSAN ALLY WA KING'S MODERN TAARABU NA HASHIM SAIDI WA MASHAUZI CLASSIC WAGOMBEA WIMBO WA..."BONGE LA BWANA", HATARIIIIII!!!.


 Msanii Hassan Ally wa King's Modern Taarabu na Hashim Saidi wa Mashauzi Classic kwa pamoja wamejikuta wakigombea jina la wimbo "BONGE LA BWANA".

Hassan Ally baada ya kutembelea mtandao wa taarabuzetu.blogspot.com na kukuta Hashim Saidi akiwaeleza mashabiki zake juu ya ujio wa wimbo wake huo mpya wa "BONGE LA BWANA", alipiga simu ofisini na kutoa malalamiko yake kwamba kichwa cha habari cha wimbo huo ni idea yake na anamshangaa Hashim Saidi kuamua kulitumia.

Anaendelea kwa kusema kwamba ana shairi ambalo kalitunga mwenyewe linaitwa BONGE LA BWANA na very soon anataka kurekodi.
 
Tulipowasiliana na Hashim Saidi alisema kwamba wimbo huo katungiwa na Thabit Abdul na tayari wamesharekodi hivi karibuni utasikika redioni hivyo kwa maelezo ya kina atafutwe Thabit Abdul, akaongezea kwamba anachojua yeye, Hassan ally anajiita Bonge la bwana tu basi na wala hajui kuhusu wimbo wa kufanana na wake.

Kwa upande wake Thabit Abdul alipopigiwa simu ili kuelezea kuhusiana na utata huu alikubali kwamba wimbo huo katunga yeye na wala sio ajabu kuona unafanana na mtu mwingine, akaongeza kwa swali kuwa mbona Shetta wa bongofleva nae katoa wimbo "Bonge la bwana"? alihoji, pia akasema kitu cha muhimu ni kwa yeye Hassan Ally kuamua kama atabadili jina la wimbo au ataendelea kulitumia! ila mimi nashauri abadiri tu.

Huu ndio mtandao makini wa taarabuzetu.blogspot.com tunachimbua habari za ndani kabisa.Usikose kufuatilia zaidi!!.