TANGAZA NASI

Kiatu Media

Feedjit

Sunday, July 7, 2013

Salha Abdallah kuanza rasmi leo kuimbia King's Modern Taarabu.

Salha Abdallah
Muimbaji Machachari Salha Abdallah aliyekuwa muimbaji wa Dar Modern Taarabu, leo hii anatarajia kuanza rasmi kuitumikia bendi yake mpya ya King's Modern Taarabu ya Jijini Dar es Salaam katika show itakayofanyika huko Kimanzichana mkoani Pwani.

Akizungumza na blog ya Taarabu Zetu meneja wa King's Abdallah Kitawine, amewaomba wapenzi na mashabiki kujitokeza kwa wingi kuja kupata burudani nzuri na ya nguvu zaidi katika utambulisho wa msanii huyo.

Salha Abdallah ni msanii aliyetokea Dar Modern Taarabu na kuhamia King's Modern Taarabu mapema wiki iliyopita.