TANGAZA NASI

Kiatu Media

Feedjit

Friday, July 12, 2013

TETESI:- HASSAN ALLY AJIUNGA NA TOT MODERN TAARAB.....

Hassanally "Baby Face".
Unaweza kuona ni kama picha ya kuigiza kwa jinsi ilivyo, mwanzoni alikuwa King's akahama akaenda T Motto, akarudi tena King's hakuishia hapo ilipoanzishwa T Motto ya awamu ya pili akarudi tena T Motto, alipoona mambo hayamuendei vyema katika bendi hiyo akaamua kurudi tena King's Modern Taarab.

Sasa tokea arudi hana hata miezi sita katika bendi hiyo, leo hii zinapatikana habari kwamba amejiunga na TOT...
Huyo ndio Young Hassan Ally "Baby face waukweli" mtandao makini wa taarabuzetu.blogspot.com ulig'atwa sikio na vyanzo vyake vya habari, ulipopata taarifa hizo haukusita kumtafuta Hassan Ally ili athibitishe juu ya habari hizo.

Alijibu hivi: "Ni kweli Kapteni Komba aliniita kwa ajiri ya mazungumzo ya kujiunga na TOT isipokuwa katika maelewano yetu kuna mambo niliyokuwa nayahitaji toka kwao ili niweze kujiunga nao hawajanikamilishia bado ila mazungumzo yanaendelea. Kwa sasa siwezi kusema nimeshajiunga nao rasmi NO!, mimi bado ni msanii wa King's Modern Taarab, Mashabiki waelewe hivyo". alimaliza kwa kusema.