TANGAZA NASI

Kiatu Media

Feedjit

Sunday, July 21, 2013

HEMEDI OMARY WA "TOT" ALALAMIKA KUTOKUWEMO KTK "TOP TEN" ZA "TAARABUZETU.BLOGSPOT.COM"...!!...


Muimbaji na mtunzi wa bendi ya taarabu ya "TOT" Hemedi Omary amelalamika kuwa kwanini yeye jina lake halikuwemo ktk orodha ya waimbaji bora kumi wa taarabu nchini?. Hemedi alitoa malalamiko yake mbele ya mwandishi wa mtandao huu akidai hajatendewa haki.

"Unajua mimi nina mchango mkubwa sana kwa hao ambao ninyi leo hii mnawaita bora! wengine nimewafundisha mwenyewe na kuwatungia karibia albam nzima, lakini ajabu mnawaita bora..!! kwa kipi haswa walichonacho!?". Alihoji kwa jazba!.

Hata hivyo sisi kama mtandao bora wa taarabu nchini tunamuomba Hemedi kupunguza jazba na kufanya kazi ili tuione na kuisikia!, katika TOP ten ya taarabuzetu.blogspot.com haimaanishi kuwa wale wote ambao hawamo hawajafikia kiwangu, waimbaji wote wapo juu ila wanatofautiana kwa namna tofauti, kuna waimbaji, watungaji, solo, bass, nk.

Hii ni kama changamoto kwa waimbaji wa Taarabu, sasa kazi buti kazi ionekane na uweze kuonekana bora kabisa, sisi mtandao wa taarabuzetu.blogspot.com tutaendelea kufuatilia na kutoa tasmini yetu kila kipindi kinapofika cha kufanya hivyo...!

0 comments:

Post a Comment