TANGAZA NASI

Kiatu Media

Feedjit

Tuesday, July 16, 2013

BAADA YA KIFO CHA MUMEWE, HADIJA KOPA AUZA GARI YAKE!!

Malkia wa mipasho nchini bibie Hadija Omary Kopa, siku chache baada ya kufiwa na mumewe kipenzi Jafari Ally, ameamua kuuza gari yake aina ya Noah...!!.

Mnyetishaji wa habari hizi aliuambia mtandao wa taarabuzetu.blogspot.com kwamba malkia aliamua kuuza gari hilo baada ya kuona linamsumbua sana na ana mpango wa kununua gari jingine, baada ya kufanikiwa kuiuza gari hiyo kwa gharama ambayo mtandao wa taarabuzetu.blogspot.com ulitajiwa.

Wakati huo huo arobaini ya mumewe Hadija Kopa, marehemu Jafari Ally ilifanyika siku ya tar 13 mwezi huu wa 7 pale nyumbani kwao Bagamoyo mtaa wa Magomeni.

Mtandao huu unawashukuru wale wote waliojitokeza katika msiba huo mpaka kumalizia arobaini. Mungu awabariki sana nyote na muwe na moyo huo siku zote.