TANGAZA NASI

Kiatu Media

Feedjit

Wednesday, July 17, 2013

HAWA NDIO WAIMBAJI KUMI BORA WA MUZIKI WA TAARABU NCHINI TANZANIA KUANZIA 2008-2013..

Taarabu ni muziki wenye asili ya pwani, na kuna taarifa zisizo rasmi ambazo zinasema muziki huu ulianzishwa miaka themanini "80" iliyopita, muziki huu umekuwa ukipitia vipindi tofauti mpaka sasa kufikia kuitwa "Modern Taarabu", kuna watu wengi maarufu walioweza kuisimamisha taarabu mpaka sasa tunaitambua kama vile Mohamedy Liasi, Abdalla Issa, Makame Faki, Siti Binti Saad na wengineo wengi shukrani ziende kwao.

Leo mtandao wa taarabuzetu.blogspot.com unawaletea majina ya wasanii kumi (10) bora ambao wamekuwa wakipendwa sana na wapenzi wa taarabu toka mwaka 2008 hadi 2013, hapa nchini Tanzania kutokana na nyimbo zao nzuri zenye ujumbe wakuelimisha na kufundisha zaidi.

"1"  Hadija Kopa = Huyu ni msanii anaekamata namba moja kwa kupendwa kulingana na kazi zake kukubalika zaidi na wapenzi wa taarabu nchini tanzania na afrika mashariki kwa ujumla, mpaka wakampachika jina "Malkia wa Taarabu Afrika mashariki na kati" kwa sasa ni mkurugenzi msaidizi wa TOT.

"2"  Isha Mashauzi = Anakamata nafasi ya pili, huyu ni Mkurugenzi wa Mashauzi Classic kwa sasa, nyota yake ilianza kuwaka baada tu ya kujiunga na Jahazi Modern Taarabu, alipotoa nyimbo yake binafsi "Nani kama mama" nje ya kundi la Jahazi ndio chanzo cha yeye kuanzisha kundi la Mashauzi Classic ambalo anaendelea nalo mpaka sasa, jambo litakalo muangusha Isha ni tabia yake ya kujisikia zaidi na kuchelewa kufika ktk matamasha yake anayoandaa au kuandaliwa!.

"3"  Bi Mwanahawa Ally = Anashika nafasi ya tatu, ni muimbaji ambae naweza kusema amepitia bendi nyingi za taarabu kuliko hawa wote kumi waliopo hapa!, Bi Mwanahawa amejaaliwa sauti nyororo tofauti na umri alionao. Kwa sasa ni msaani wa 5 Stars lakini ukienda pale lango la jiji katika show ya East African Melody utamkuta anaimba...
Huyo ndio bi Mwanahawa Ally na falsafa zake za pesa kwanza......!

"4"  Sabaha Salum Muchacho = Ni mama wa makamo aliejaaliwa uzuri, ukimuona anavyojipenda na alivyo na sura nzuri unaweza kudhania binti kumbe lah! Mara kwa mara show zake hufanya Muscat na Oman!, ni ngumu kumkuta Sabaha ktk show za vichochoroni kwa ufupi anaijua thamani yake, anashika nafasi ya nne!.
"5"  Zuhura Shabban = Kwa sasa maskani yake ni Unguja na anamiliki chuo cha kuwafunza watu jinsi ya uimbaji bora wa Taarabu. Pia ni msaani wa Taarabu pekee anae endesha gari la thamani kubwa kuliko yeyote yule. Ana nyimbo nyingi nzuri ambazo aliziimba akiwa na Zanzibar Stars na mpaka sasa zinatamba. Anashika nafasi ya tano.
"6"  Mzee Yusuph = Ametokea mbali kimuziki mpaka kufikia kumiliki bendi yake mwenyewe ya Jahazi. Yeye ni miongoni mwa waanzilishi wa Zanzibar Stars miaka kadhaa iliyopita. Ni msaani wa kiume muimbaji ambae hana mpinzani kwa sasa.
Kasoro ya mzee Yusuph ni mwiko kwake kupiga picha na shabiki yeyote pindi anapokuwa steji... Mmh! hii balaa!, anashika nafasi ya sita!.

"7"  Jokha Kasim = Huyu ametoka katika familia ya waimbaji haswa kwani ana wadogo zake watano wote ni waimbaji wa Taarabu. Kwa sasa yupo T MOTTO na ana nyimbo inayotisha kwa sana katika vituo vya redio ya "Domo la udaku".
Inasemekana ni mama Mkurugenzi wa T MOTTO kwa sasa yaani usingizi wa Amin Salmin... Upo hapo!.
"8"  Omary Tego = Wengi wanasema ana fanana kila kitu na Mzee Yusuph, hadi uimbaji... Huyu ni Omary Tego Mkurugenzi wa Coast Modern Taarabu.
Wakati inaanzishwa 5 Stars ya Shark's, wasanii wake wawili ambao ni ndugu zake walimhama nao ni Maua Tego na Yusuph Tego, lakini yeye hakukata tamaa akaendelea na kutoa wimbo uitwao "Surprise"!! Ni balaah!.

"9"  Hassan Ally = Historia yake ameanzia madrasa kuimba kaswida, mpaka kuingia kwenye muziki wa mwambao. Hassan Ally ni muimbaji na pia ni mtunzi mzuri sana wa mashairi ya Taarabu. Kwa sasa ni msanii wa King's Modern Taarabu japo kuna fununu kwamba anatakiwa na Kapteni Komba pale TOT Taarabu!.
"10"  Ahmed Mgeni = Ni msaani wa Zanzibar One kwa sasa chini ya mkurugenzi wake Ally Ngereja. ametokea mbali katika muziki huu wa taarabu mpaka hapo alipo. Kuna kipindi alikutana na Hassan Ally pale New Zanzibar ikasemekana Hassan Ally aliamua kuhama bendi kwa kuogopa uwezo wa Ahmed Mgeni atamfunika. Siku moja watatuambia je ni kweli haya?.
Kwa sasa Ahmed Mgeni yupo kwao Zanzibar anasumbuliwa na maradhia, inshallah Mungu amjaalie apone.
Huyo ndio Ahmed Mgeni mzee wa "Sitetereki".

Tathimini hii ni kwa niaba ya mtandao wa taarabuzetu.blogspot.com na sivinginevyo!!.