TANGAZA NASI

Kiatu Media

Feedjit

Sunday, July 28, 2013

HATIMAE SHOMARI ZIZZOU "BABU" ASAINI 5 STAR'S MORDEN TAARABU.

Shomary-Zizzou-(Babu)

Wahenga wanasema kuwa ukisema cha nini, wenzio wanasema watakipata lini, 

Yule mpiga gitaa la besi maarufu katika tasnia ya Taarabu nchini Tanzania Shomari Zizzou au "Babu" jana Jumamosi muda wa saa 11 jioni alisaini rasmi mkataba wa kuitumikia bendi ya 5 Stars Modern Taarabu.

Akizungumza na mtandao makini wa taarabuzetu.blogspot.com mkurugenzi wa 5 Stars Mr Shark's alisema kuwa Shomari Zizzou ni msaani wao rasmi kwa sasa na atasaidiana katika besi na Shabban Kondo. Pia wana mipango ya kuongeza waimbaji wawili maarufu hapo baadae, Mr Sharks alisema. 
Shomari alipunguzwa na Jahazi Modern ndo akawa huru kwenda bendi yoyote na hatimae kuangukia mikononi mwa 5 Stars.

0 comments:

Post a Comment