TANGAZA NASI

Kiatu Media

Feedjit

Tuesday, July 9, 2013

OMARY TEGO: COAST MODERN TAARAB HAIJAFA NA HAITOKUFA DAIMA!!.


Mkurugenzi na Muimbaji mkongwe wa musiki wa mwambao Tanzani wa Coast Modern Taarab, Omary Tego ameuambia mtandao wa taarabuzetu.blogspot.com kwamba bendi yake haijafa wala haitokufa.

Msanii huyo mwenye mashairi matamu ameendelea kusema ukimya wao ni kwasababu wanajipanga kufanya mambo mazuri zaidi, hivi karibuni bendi ya Coast iliondokewa na wasanii wake wanne maarufu khali iliyopelekea kuyumba kidogo.

Wasanii walioondoka ni Maua tego na Yusuph tego wapo 5Stars Modern Taarab, Kibibi Yahya yupo King's Modern Taarab na Asia Mariam yeye yupo Gusagusa Min Bendi zote za Dar es Salaam.

Mwezi uliopita Omary tego alitoa wimbo mpya kabisa uitwao "Surprise" ili kuwafahamisha wapenzi na mashabiki wake kwamba Coast ipo na itaendelea kuwepo. Coast Modern Taarab ni moja kati ya bendi bora kabisa za taarabu hapa nchini!!.

Omary Tego alipoulizwa kuhusiana na kuhamia katika Bendi nyingine iliyopo Dodoma, alikanusha kuwa yeye ni Mkurugenzi wa Coast Modern Taarabu, hawezi kuiacha Bendi yake na kwenda kujiunga na Bendi nyingine.

Wapenzi wote wa burudani hasa wale wa Coast Modern Taarabu msidanganyike Bendi ipo imara tunawaandalieni mambo mazuri "Omary Tego".