TANGAZA NASI

Kiatu Media

Feedjit

Wednesday, July 24, 2013

KING'S WAINGIA KAMBINI LEO JUMATANO, KUTENGENEZA MBILI KALI...

Aisha Vuvuzela
Salha Abdallah
Bendi ya King's Modern Taarabu, leo hii Jumatano wanaingia kambini tayari kwa maandalizi ya nyimbo zao mbili mpya kabisa.

Director wa King's Modern alizungumza na mtandao wa taarabuzetu.blogspot.com na kusema nyimbo hizo zitaimbwa nao Aisha Vuvuzela na Salha Abdallah, wote hawa ni wasanii wapya katika kundi hilo.Director Alhaji Kijoka aliwaomba wadau na wapenzi wa bendi hiyo kujiandaa kusikia kazi nzuri toka kwao kwani mara kwa mara wamekuwa hawabahatishi wanapoamua kufanya jambo. 

Aisha Vuvuzela hapo kabla alikuwa katika bendi ya Mashauzi nae Salha Abdallah alikuwa Dar Modern Taarabu. 
Sisi kama mtandao makini tunasubiri kusikia kazi nzuri kutoka kwa wasanii hao wakali kabisa.

0 comments:

Post a Comment