TANGAZA NASI

Kiatu Media

Feedjit

Thursday, July 11, 2013

HAKIM SHAFII:- MARUFUKU KWA YEYOTE KUTUMIA JINA LA ZANZIBAR STARS!!.


Mkurugenzi wa Zanzibar Stars Modern Taarab Hakim Shafii, ameongea na mtandao makini wa taarabuzetu.blogspot.com na kutoa onyo au kalipio kali sana kwa yeyote anaetumia jina la Zanzibar Stars Modern Taarabu kujinufaisha pasipo idhini yake yeye mwenyewe.

Unajua ndugu mwandishi kuna watu ambao nisingependa niwataje kwa majina wamekuwa wakilitumia jina la bendi yangu pasipo idhini yangu. Tena wanadiliki hata kuokoteza-okoteza wasanii waliowahi kupigia Zanzibar Stars zamani na kusafiri nao mikoani kwenda kufanya show, mimi kama mmiliki halali nakemea sana jambo hili na sitaki kuona linatokea tena.

Mimi Hakim shafii ndio mmiliki halali wa Zanzibar Stars na wala sivinginevyo, alimalizia.

Zanzibar Stars ni bendi kongwe ya Taarabu ambayo imetoa vipaji vingi vya waimbaji maarufu kama Jokha Kassimu, Mzee Yusuph, Zuhura Shabban na wengineo wengi.