TANGAZA NASI

Kiatu Media

Feedjit

Thursday, July 11, 2013

TETESI TOKA 5 STARS:- ZENA MOHAMEDY APOKONYWA WIMBO BAADA YA KUTOFAUTIANA NA UONGOZI....!

Mariam BSS.
Kuna tetesi zimelifikia dawati letu la habari hapa katika mtandao wa taarabuzetu.blogspot.com.

Taarifa hizo zinasema msanii wa siku nyingi Zena Mohamedy ametofautiana na uongozi wake wa 5Stars Modern Taarabu mpaka kufikia kupokonywa kabisa wimbo na kupewa mwimbaji mwingine Mariam BSS ambaye aliuimba.

Wimbo huo umetungwa nae El-Hatibu unaitwa: "Jibu ninalo nasubiri uropoke" ni moto wa kuotea mbali kwani kila unapopigwa stejini hakuna mpenzi anaekaa bila kucheza. Kwa mujibu wa chanzo chetu cha habari toka humo humo 5Stars.

Zena alitofautiana na viongozi wake wakati wapo Mtwara katika show zao!.
Huyu dada ni jeuri sana kwakweli... Sijui anajivunia nini tu maana.... Mtandao wa taarabuzetu.blogspot.com ulimtafuta zena ili kuthibitisha hili lakini alipopokea simu alianza kutoa maneno machafu wala yasiyo na stara kwa mwandishi!.

Sisi kama wadau wakuu wa Taarabu Tanzania tunamkumbusha kwamba msanii ni kioo cha jamii hivyo kuwa makini sana, ni vyema ukaongea na kutoa ya Moyoni ili Jamii ijue!!.