TANGAZA NASI

Kiatu Media

Feedjit

Thursday, July 11, 2013

HANIFA MAULIDI "JIKE LA CHUI";- SIPO, TOT WALA KING'S MODERN TAARABU KWA SASA.....!


 Muimbaji wa taarabu anaekuja kwa kasi ya ajabu kwa sasa Hanifa maulidi "Jike la Chui" amefunguka "live" mbele ya mtandao makini wa taarabuzetu.blogspot.com

Hanifa alisema yeye kwa sasa ni msanii huru hana bendi na yeyote mwenye kisu kikali anaweza kumvuta katika bendi yake na wakafanya kazi, kikubwa ni maslahi yawe mazuri kwake hakuna shida.

Alipoulizwa kwamba kuna habari zimezagaa mjini kwamba yeye kwa sasa yupo TOT, alisema ni kweli nafanya kazi na TOT lakini si mwajiliwa wa TOT kifupi sina mkataba nao ila kama wakinipa mkataba na tutaelewana na uongozi nitasaini hakuna shida.

Hanifa ambae kwa sasa anatamba na nyimbo yake ya "Makavu live" amewaomba mashabiki wake kusubilia video ya wimbo huo ambayo anatarajia kufanya na kampuni ya Thabit abdul iitwayo "Soweto Picture Production".

Hanifa pia ameweza kufanya kazi na bendi za King’s Modern na Mashauzi Classic.