TANGAZA NASI

Kiatu Media

Feedjit

Sunday, July 14, 2013

ABDUL MISAMBANO AMFUNIKA DOCTOR KIFIMBO NDANI YA CLUB LAAZIZI DODOMA...!!

Abdul Misambano
Abdul Misambano ni msanii maarufu sana katika tasnia ya Taarabu hapa nchini Tanzania, kwa sasa Misambano ni mwajiriwa wa TOT TAARABU yenye maskani yake maeneo ya Mwananyamala "A" Dar es Salaam.

Siku ya tar 5 mwezi wa saba aliandaa tamasha la taarabu huko Dodoma ndani ya ukumbi wa Club Laazizi na wasanii waliokuwepo katika onyesho hilo ni pamoja na Bi Mwanahawa Ally, Jokha Kasimu, Bi Rukia Juma Aziza Bonge na wasanii wengine wengi.

Lakini hapo kabla Muheshimiwa Doctor Kifimbo mkurugenzi wa Kifimbo FM Dodoma nae aliandaa tamasha la Taarabu ndani ya ukumbi huo huo siku ya ijumaa tar 28 mwezi wa 6 ambalo halikufanya vizuri kama lile la Abdul Misambano, jambo lililotafsiriwa na mashabiki kwamba safari hii Doctor Kifimbo kafunikwa na Abdul Misambano live bila chenga kwa mchuano usio rasmi!.

Katika show ya Doctor Kifimbo wasanii waliokuwepo stejini ni pamoja na Hassan Ally, Issa Kamongo, Omary Tego na wengineo.

Sisi mtandao wa taarabuzetu.blogspot.com tunatoa pongezi kwa Abdul Misambano na muheshimiwa Kifimbo kwa kuonyesha kuwajari wakazi wa Dodoma na kuwapelekea burudani za Taarabu mara kwa mara!!.