TANGAZA NASI

Kiatu Media

Feedjit

Sunday, July 7, 2013

Off - Side Trick yapagawisha Bukoba.


Kundi la Off-Side Trick la Jijini Dar es Salaam limefanya show kabambe na kuchengua mashabiki waliofurika kwa wingi katika Ukumbi wa Linaz Club Bukoba na show ya pili walipiga Muleba ilikuwa show nzuri sana wakitumia mtindo wao maarufu wa Mduara.

Katika show hiyo walipiga nyimbo zao karibu zote zilizotamba kama: Samaki, Ahmada, Kidudu Mtu Pamoja na Nyimbo zao za hivi karibuni kama: Usinipe na Nipe Nikupe.

Akizungumza na Mtandao wa Taarabuzetu.blogspot.com msanii wa kundi hilo Hammer Q, amesema wamefurahishwa na mapokezi ya huko na siku moja watarudi kufanya show.

Alisema leo wanatarajia kurudi jijini Dar es Salaam.